Sunday, 6 May 2018

Mbeya Press Club ilivyoadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari

Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika akizungumza wakati akifungua mkutano wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club) unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo yanafanyika kila mwaka Mei 3. Wanahabari mkoani Mbeya wamadhimisha siku hiyo leo.

Kutoka kulia ni Frank Leonard mwenyekiti wa Press Club Iringa, Modest Nkurlu mwenyekiti wa Mbeya Press Club na kushoto ni Fredy Jackson kaimu katibu mkuu Mbeya Press Club. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mkoa wa Mbeya ni "Uhuru wa Vyombo vya habari ni chachu ya uwajibikaji kwa maendeleo ya mkoa wa Mbeya". 

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Paul Ntinika wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Frank Leonard mwenyekiti wa Iringa Press Club wakati akizungumza katika mkutano huo kama mmoja wa wageni waalikwa, katikati ni Modest Nkurlu mwenyekiti wa Mbeya Press Club na kushoto ni Fredy Jackson kaimu katibu mkuu Mbeya Press Club.


Frank Leonard mwenyekiti wa Iringa Press Club akichangia mada katika mkutano huo.


Naibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Mbey, Julieth Godrey akichangia na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu taasisi hiyo na jinsi wanahabari wanavyoweza kushirikiana nayo.


Mwanahabari Charles Mwakipesile na baadhi ya wenzake wakiwa katika mkutano huo unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.


Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mjadala huo.


Mmoja wa wadau wa wanahabari, Joseph Mwaisango aliyeshiriki katika maadhimisho hayo.

Wadau mbalimbali wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo.

Mwanahabari Naomi Malala akizungumza jambo na mwenzie Rachel Mwangosi huku Plaxeda Mbullu akiwasikiliza.


  
Keneth Simbeye Rais mstaafu wa Vyama vya waandishi wa habari nchini (UPC) pamoja na washiriki wengine wakiwa katika mkutano huo.


Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari mara baada ya kufungua mkutano wa Chama chao mkoani Mbeya (Mbeya Press Club) unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Mkapa jijini humo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo yanafanyika kila mwaka Mei 3.

No comments:

Post a Comment