Tuesday, 22 May 2018

Mbono mmea unaotibu miguu kuwaka moto


Mbono
SI jambo la kushangaza nyakati hizi kukuta mlundikano mkubwa wa wagonjwa wa rika zote katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zetu hapa nchini.

Mlundikano huo unatoa taswira kuwa watu wengi wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali yanayohitaji tiba, huku yale yasiyoambukiza nayo yakishika kasi.

Zamani watoto waliokuwa wakizaliwa kabla ya wakati walikuwa wakizikwa ndani ya eneo lenye migomba. Eneo hilo na hata baadhi ya maeneo ya makaburi waliyozikwa watoto watu wamekuwa wakihadhalishwa kutoyakanyaga ili kuepukana na matatizo hayo.

Mafuta ya mbono ni dawa kwa kuwa yanasaidia kuondoa maumivu ya miguu kuwaka moto inayotokana na sababu hizo na nyingine. Chukua majani ya nchani ya mbono yapike kisha kanda eneo lenye mauamivu halafu paka mafuta yake.

Tiba hii pia inatibu hata maradhi ambayo yamesababishwa na hasidi. Mmea huu pia hutumika katika masuala mazima ya uzazi wa mpango.

Mbono ni mmea wa kupandwa lakini pia unaweza kuota wenyewe sehemu yoyote, hata kama ni kwenye eneo la pori karibu na makazi ya watu.

Mmea huu ambao ni tiba kuanzia mafuta yanayotokana na mbegu, majani na mizizi unatumika tangu enzi za mababu kutibu maradhi mbalimbali ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Mchanganua huu kwa ufupi umeletwa kwako na mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai, kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea wavuti yetu kwa anuani ya www.dkmandai.com.

No comments:

Post a Comment