Sunday, 27 May 2018

Mdalasini suluhisho la ugumba na utasa


Magome na unga wa mdalasini

MDALASINI ni kiungo kinachoongeza ladha nzuri katika vinywaji na vyakula.
Wakulima hustawisha mdalasini kama zao la biashara ambapo wanaweza kupata mavuno mengi na bora iwapo watazingatia kanuni na taratibu za kilimo hicho.
Visiwa vya Zanzibar ni maarufu zaidi kwa kilimo cha zao hili. Mti wa mdalasini tangu upandwe unaweza kudumu kwa zaidi ya miaka 20. Magome hutumika kama kiungo, majani yake hutumika kutengenezea mafuta.
Kitiba mmea huu una faida nyingi kwa kuwa unatibu magonjwa mengi. Unaondoa ugumba kwa mwanaume na utasa kwa mwanamke.
Mwaume atumie vijiko viwili vya unga wa magome ya mdalasini achanganye na asali katika mlo wa jioni. Kwa mwanamke inaimarisha na kuhamasisha kizazi.
Kwa wale tasa  watumie kipimo cha mwanaume kila siku kwa miezi kadhaa wataona mujiza ukifanyika.
Tumia vijiko viwili vya asali na vitatu vya unga wa mdalasini koroga pamoja kwenye maji moto na kunywa itaondoa asilimia 10 ya lehemu (chorestrol) mwilini mwako. 
Kwa maradhi ya mafua tumia kijiko kimoja cha chai cha asali na kingine cha unga wa mdalasini mara mbili kwa siku muda wa siku mbili, mafua na kikohozi vitaondoka.
Tatizo la kunyonyoka nywele, tumia kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na kingine cha asali na kingine kidogo cha mafuta ya mzeituni changanya pamoja, paka kichwani viache kwa muda wa robo saa kisha osha kichwa.
Endelea mara moja kwa siku, kila siku utaona mtokeo.
Mdalasini pia unazuia na kuondoa au kufukuza gesi tumboni, kutia joto tumbo lililopoa, vidonda vya tumbo, kichefuche na kutapika na kuharisha.
Mmea huu pia unasaidia kusukuma mbele muda wa kuingia katika hedhi baada ya kujifungua. Siku ya kujifungua tafuna kipande cha mdalasini mfululizo kwa muda wa siku 30 utachelewa kuingia hedhi kwa muda wa mwaka na nusu au miaka miwili na hivyo itazuia usipate mimba kwa wakati usiotakiwa. 
Mada hii imeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.
Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

1 comment: