Saturday, 5 May 2018

Menejimenti ya mahakama ya Tanzania yawaaga majaji wapya walioteuliwa kutoka mahakama

Majaji wapya wa mahakama kuu walioteuliwa kutoka mahakama wakiwa katika picha ya pamoja, katikati ni Ilvin Mugeta, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kushoto ni Elinaza Luvanda, jaji wa mahakama kuu ya Tanzania na aliyesimama kulia ni Mustapher Siyani, jaji wa mahakama kuu ya Tanzania, Majaji hawa wameagwa rasmi mapema jana Mei 04, 2018 na Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania.


Sehemu ya wajumbe wa menejimenti ya mahakama ya Tanzania wakiwa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa maktaba-mahakama ya rufani, katika kikao hicho wajumbe hao walipata fursa ya kuwaaga waliokuwa wajumbe wa menejimenti ambao waliteuliwa hivi karibuni kuwa majaji wa mahakama kuu ya Tanzania, walioketi mbele (katikati) ni mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni mtendaji mkuu wa mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga, kulia ni mwenyekiti mwenza wa kikao hicho ambaye pia ni msajili mkuu-mahakama ya Tanzania, Katarina Revocati na kushoto ni msajili-mahakama ya rufani, John Kahyoza.


Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta (aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa menejimenti, katika salamu zake za shukrani, Jaji Mugeta ameishukuru menejimenti kwa ushirikiano katika kipindi chote alichofanya kazi katika nafasi ya msajili-mahakama kuu, aidha ameomba ushirikiano zaidi katika nafasi hii mpya.


Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania,  Elinaza Luvanda akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa menejimenti, amemshukuru Rais na viongozi wengine wa mahakama kwa uteuzi wa nafasi hiyo, na ameahidi kutoa ushirikiano katika kazi yake.


Mwenyekiti wa kikao cha menejimenti ya mahakama ambaye pia ni mtendaji mkuu wa mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kushoto) akikabidhi zawadi ya nakala za vitabu vya mpango mkakati wa mahakama ya Tanzania, kwa jaji wa mahakama kuu, Ilvin Mugeta (kulia), anayeshuhudia mchakato huo (katikati) ni msajili mkuu- mahakama ya Tanzania, Katarina Revocati.


Mwenyekiti wa kikao cha menejimenti ya mahakama ambaye pia ni mtendaji mkuu wa mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kushoto) akikabidhi zawadi ya nakala za vitabu vya mpango mkakati wa miaka mitano wa  mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) kwa Jaji Elinaza Luvanda (kulia) anayeshuhudia ni msajili Mkuu- Mahakama ya Tanzania, Katarina Revocati.


Jaji Elinaza Luvanda (kulia) akipeana mkono na msajili wa Mahakama ya Rufani (T), John Kahyoza (kushoto) mara baada ya kupokea nakala zake za mpango mkakati wa mahakama ya Tanzania.


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapher Siyani (kulia) akipokea nakala ya kitabu cha mpango mkakati kutoka kwa mtendaji mkuu mahakama (kushoto).


Picha ya pamoja ya majaji na wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania, aliyeketi katikati ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta, wa pili kushoto ni Elinaza Luvanda, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa pili kulia ni Mustapher Siyani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania na wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania.
(PICHA NA MARY GWERA, MAHAKAMA)

No comments:

Post a Comment