Wednesday, 30 May 2018

Mganga mfawidhi Kakonko ajinyoga


Rhoda Ezeikel, Kigoma

MGANGA mfawidhi wa kituo cha afya Kakonko, Kigoma, Dk. Mejo Banikila ( 43 ) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia taulo.
Mkuu wa wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala amethibitisha hilo linalodaiwa kutokea usiku wa kuamkia jana.


Kanali Ndagalla amesema matukio ya watu kujinyonga katika wilaya ya Kakonko yamekuwa yakiongezeka na wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.

Aidha, mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kuhudhuria kanisani na misikitini ili kusikiliza mahubiri yatakayosaidia kupunguza msongo wa mawazo unachangia kuchukua uamuzi kama huo.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Martin Otieno alithibitisha kutokea tukio hilo na kuwaomba wananchi kuacha kuchukua maamuzi ya kujinyonga.

Kwa upande wao baadhi ya wapangaji wenzake wamesema kwa muda wa miezi minane wameishi naye vizuri licha ya kuwa siku mbili kabla ya tukio amekuwa akionekana mnyonge.

Wamesema wakati wa uhai wake Banikila alikuwa akifanya kazi zake vizuri na alikuwa akijitoa kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma kwa wakati na kwamba watamkumbuka kwa mambo mengi.

No comments:

Post a Comment