Friday, 11 May 2018

Mgogoro wa ardhi wa wakazi Pugu Kinyamwezi wapatiwa ufumbuzi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa eneo la Pugu Kinyamwezi lenye ukubwa wa hekari 40 ambalo mmiliki wake ni Jeshri Rawel (kulia kwa waziri) ambaye anadai kuvamiwa na wakazi hao.


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  William Lukuvi ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu kati ya wakazi wa eneo la Pugu Kinyamwezi na mmiliki wa eneo hilo, Bibi Jeshri Rawel.

Waziri Lukuvi ametoa uamuzi wa kuwataka wakazi wa eneo hilo ambao wamejenga katika shamba la mmiliki huyo lenye ukubwa wa hekari 40 na kuweka makazi yao kulipia gharama za umilikishwaji ardhi ili waweze kupatiwa haki ya kumiliki eneo hilo.

No comments:

Post a Comment