Tuesday, 22 May 2018

Mikoko ni tiba kwa mama mwenye tatizo la uzazi


Mikoko

MIKOKO ni mimea inayoota pembezoni mwa bahari ambayo inasaidia kupendezesha mandhali ya bahari eneo inayoota.

Mara nyingi eneo la mikoko lisipoharibiwa linaongeza mvuto kwa watu wanaotembelea fukwe za bahari kwa kuwa linakuwa na hewa safi inayovutia mtu kuendelea kukaa.

Hata hivyo, mmea huu tangu enzi za babu zetu ni dawa inayotibu maradhi mengi.

Mizizi ya mikoko ikichemshwa na ubani wa mashtaka pamoja na kuku jike mwenye umri wa zaidi ya mwaka mmoja mchuzi wake akinywa  mwanamke ambaye ana amini hazai kwa sababu ya kufungwa na nguvu za giza atazaa watoto wake.

Pia mtu anayesumbuliwa na tatizo la kifua kikavu, maradhi ya moyo na athma achemshe gome la mkoko anywe kikombe chai kimoja asubuhi na jioni.

Majani ya mkoko yaliyokaushwa kivulini na kupatikana na unga wake, yanasaidia kukoma hedhi kwa kinamama wenye tatizo la kuendelea hedhi licha ya kuwa na umri mkubwa.

Mchanganua huu kwa ufupi umeletwa kwako name mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu www.dkmandai. com.

No comments:

Post a Comment