Saturday, 19 May 2018

Mkaa unasaidia kuondoa tatizo la kifafa cha mimba


Mkaa
LICHA ya mkaa kutumika kupikia vyakula na mambo mengine, nishati hii ni tiba kwa maradhi mbalimbali kwa kuwa ni mkusanyiko wa aina nyingi za miti ya porini.

Mkaa unasaidia kuzuia kutapika na kuharisha, kutibu maradhi ya kifafa cha mimba na kumwepusha mjamzito anayetarajia kufanyiwa upasuaji.

Chukua mkaa wa mkwanga na ule wa kifuu cha nazi saga pamoja kisha weka kwenye uji mwepesi kijiko kimoja cha chai kunywa asubuhi na jioni  utaondokana na tatizo la kifafa cha mimba na kuzaa kwa oparesheni.

Kwa anayeharisha au kutapika achukue mkaa unatumika kupikia ausage unga wake autumie katika maji moto au uji mwepesi tatizo hilo litamwondoka.

Kwa mama anayetaka kufanyiwa upasuaji wa uzazi, dawa hii itamwongezea nguvu ya kusukuma mtoto na kudhibiti mapigo ya moyo yanayokwenda kasi na kubaki katika hali ya kawaida.

Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au nipigie simu kwa namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment