Wednesday, 16 May 2018

Mkomamanga mti wa kiimani unaosaidia kupambana na maradhi mengi


Sehemu ya mti wa komamanga (mkomamanga)

KOMAMANGA siyo tunda maarufu sana hapa nchini, licha ya kuwa lina faida nyingi kwa afya ya binadamu.

Mkomamanga ambao asili yake ni Asia na India unasaidia sana wenye matatizo ya vidonda vya tumbo na kinamama wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.

Juisi ya tunda la komamanga lenye mbegu nyingi na linalofanana na pera kwa kiasi, inaponywewa kulingana na maelekezo ya kitiba husaidia kuondoa matatizo hayo.

Mizizi ya mkomamanga inapochemshwa na maji yake kunywewa na mwenye matatizo ya mgolo inasaidia kuondokana na tatizo hilo.

Kiimani mmea huu ukipandwa nyumbani huleta wageni wema na kuzuia kuja watu waovu kama wezi na wachawi, ni mti mlinzi katika jamii.

Mchanganua huu umeletwa kwako na mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.
Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana na mtaalam Mandai kwa simu namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment