Thursday, 17 May 2018

Mtunguja mmea unaosaidia tatizo la vikanga , vikangoMTUNGUJA (mti wa tunguja) ni mmea unaofanana na nyanyachungu, ikiota pamoja shambani ni vigumu kuitofautisha.

Unasaidia kupambana na maradhi mbalimbali ikiwemo vikanga, vikango, bawasili, kichwa, kizunguzungu na ngili.

Kwa anayesumbuliwa na vikanga (vipele vinavyoota kuzunguka sehemu ya haja ndogo) na vikango (vipele vinavyoota sehemu ya haja kubwa) chukua matunda ya tunguja weka katika sufuria au chungu funika vizuri kuzuia mvuke baada ya kuweka maji yachemshe.

Baada ya kuipua, chukua meza ilaze upande mmoja juu ya dawa hii kisha kaa ukiwa hujavaa nguo ya ndani ili mvuke uingie katika sehemu ya haja kubwa au ndogo ikiwa unakabiliwa na matatizo hayo.

Wakati huo uwe umejifunika kwa nguo nzito. Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili. Kama huna stuli toboa kiti cha kukalia jikoni kisha kiweke juu ya dawa baada ya kuifunua kaa hapo ili mvuke kupitia tundu hilo ukupate.

Mizizi ya tunguja pia inasaidia kupambana na maradhi ya ngili, hivyo ichukue kiasi cha kujaa mkono, ioshe vizuri kisha ichemshe na kunywa maji yake.

Majani ya tunguja pia yanasaidia tatizo la kipanda uso, yachemshe na kisha jifushe kama nyungu yanasaidia kuondoa kipanda uso na homa za mara kwa mara.

Ukiponda majani yake na kupata unga utumie katika maji moto au uji mwepesi, unasaidia kwa wenye tatizo la kutapika na kuharisha.

Mchanganua huu umeletwa kwako na mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana na mtaalam Mandai kwa simu namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment