Tuesday, 8 May 2018

Mwinga jini inasaidia watu wanaochelewa kupata watoto                          Mwinga jini

UTAJIRI wa mimea asili umeendelea kuwa na tija kubwa katika jamii zetu siku hadi siku.

Mimea hii licha ya kupendezesha mazingira, kutumika kama kuni, mbao kwa ajili ya kuezekea nyumba zetu, pia ni tiba nzuri ambayo ni asili yetu Waafrika.

Tunayo aina nyingi mno ya mimea ambayo hadi sasa bado idadi yake haijajulikana inayotumika kwa matumizi mbalimbali katika jamii zetu.

Mwingajini ni moja ya mimea muhimu mno kwa maisha ya jamii zetu zamani, sasa na hata siku zijazo.

Mti huu mara nyingi unaota pembeni ya nyumba au katika maeneo ambayo watu wamehama.

Mti huu ambao unaweza kupandwa pia una  faida nyingine kwa binadamu ambayo ni kuponya tatizo la ugumba kwa kinamama na kinababa ambao wanachelewa kupata watoto.

Wenye tatizo hilo wakipatiwa maelekezo ya kitaalamu ya namna ya kutumia dawa hii wanaweza kuzaa bila shida.

Mti huu una uwezo mkubwa wa kubadilisha mwili wa mwanamke na mwanaume kwa kupevusha mayai na mbegu za kiume na hivyo kuwezesha uzazi kwao.

Pia kwa wale wanaoshindwa kupata watoto baada ya kukumbwa na nguvu za giza mti huu una saidia.

Wakati wa kutumia unaweza pia kuchanganya na miti mingine kama pangaa na mlangamia.

Matumizi ya dawa hii yanafanyika sanjari na kunywa supu ya kuku jike mwenye umri wa zaidi ya mwaka mmoja.

Naweza kusema kuwa dawa hii ni tiba nzuri kwa magonjwa ambayo yameshindikana hospitalini.

Kwa mwenye tatizo asisite kuja makao yetu makuu ambapo utapata maelezo ya kina ya namna sahihi ya kutumia mmea huu kuondokana na tatizo lako la uzazi.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment