Friday, 25 May 2018

Nazi huchochea afya kwa wazee na watoto


Nazi
ZIPO aina nyingi za tiba asili zinazosaidia kupambana na maradhi mbalimbali tangu enzi za mababu ambazo tunaendelea kuzitumia hadi sasa.  

Tiba za mizizi, matunda na magome zimeonesha uwezo mkubwa wa kuyakabili maradhi mengi yakiwemo yale yanayoshindikana katika tiba za kisasa.

Nazi ni kiungo  lakini pia ni tunda maarufu hususan kwa wenyeji wa mikoa ya Pwani kuliko wale wa mikoa ya bara. Kiungo hiki kilichosheheni asidi ya laurik kina uwezo wa kupambana na fangasi na virusi vya Ukimwi.

Asidi ya laurik hupambana sio tu na virusi vya Ukimwi bali pia na bakteria na maradhi ya ngozi na mengine.

Nazi changa (dafu) inapoliwa huleta afya mwilini hasa kwa wazee na watoto, huchochea afya ya damu, huimarisha utumbo, hufanya viungo viwe na nguvu na hukomesha maradhi ya kuwaka tumbo.

Pia husaidia homa ya nje na ndani, husaidia tatizo la kupungua uzito, magonjwa ya neva na pia kuchoka kwa neva, huondoa na kusaidia uchovu wa mwilini na husaidia pia kukomesha usahaulifu.

Nazi ina vitamini A, B na E kwa wingi. Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu, www.dkmandai.com ili kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu afya zetu.

No comments:

Post a Comment