Friday, 4 May 2018

Ndimu, tangawizi vinasaidia kuondoa gesi tumboniZIPO sababu nyingi zinazofanya chakula kishindwe kuyeyushwa ndani ya tumbo la binadamu na hivyo kuwa kiini cha matatizo mbalimbali ikiwemo maumivu ya tumbo.

Kula kupita kiasi, kula mara kwa mara hata kama huna njaa, kula kwa haraka bila kutafuna sawasawa na kutokuwa na muda rasmi wa kula  chakula.

Unapogundua kuumwa tumbo, kichefuchefu, kujamba, kuharisha na tumbo kujaa hewa mara nyingi vinaweza kusababishwa na mfumo wa uyeyushaji chakula kuwa na hitilafu.

Ukiona tatizo hilo unaweza kutumia ndimu, tangawizi, kitunguu swaumu, msubili, komamanga na asali kwa kuwa vinasaidia kuondokana na tatizo hilo.

Ndimu na tangawizi

Kijiko kimoja cha juisi ya ndimu, changanya na kingine chenye ujazo huo cha tangawizi, kunywa mara tatu kwa siku kama tiba ya kujaa tumbo.

Kitunguu swaumu

Chukua punje 20 za kitunguu swaumu saga, tia katika nusu glasi ya maziwa, koroga vizuri, kunywa vijiko viwili vya mezani robo saa kabla ya kila mlo mkuu kwa siku. Tunza ndani ya freji kiasi cha mchanganyiko huo kinachobaki.

Msubili

Jani la msubili kata kipande cha nusu futi, kate vipande vidogo vidogo kula kama kachumbari.

Komamanga na asali

Juisi ya komamanga, changanya na kijiko cha asali, kunywa kwa ajili ya kutibu tumbo kujaa, tumia tiba hii mara mbili kwa siku kwa muda wa siku tatu.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment