Monday, 28 May 2018

Papai jekundu linasaidia wanaosumbuliwa na tatizo la kutopata choo


Papai jekundu

KWA kawaida mwanadamu anakwenda haja kubwa mara mbili au tatu kwa siku. Mara nyingi inakuwa saa mbili hadi nne baada ya kula mlo iwe asubuhi, mchana au jioni.

Hiyo inakuwa baada ya tendo la usanisi wa chakula tumboni kukamilika. vinginevyo kinyesi hicho kisipotoka kinageuka sumu na ambayo inaweza kumsababishia mtu matatizo ya vichomi na mate mazito mdomoni.
Shirika la Afya Duniani (WHO), linasema asilimia 80 ya maradhi yanayomkabili binadamu yanasababishwa na vyakula anakula kila siku.
Hivyo, leo nimeona niwaeleze japo kwa ufupi namna ya kufanya iwapo utakumbwa na tatizo hilo.
Chukua papai jekundu ndani, kata vipande viwili, kimoja miongoni mwavyo kikatekate changanya na ndimu au limau kula kila jioni mchanganyiko huo wa vipande.
Papai hili linasaidia sana tatizo hilo kwa sababu lina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi (fible),  zinki na vitamin C kwa wingi ambapo ukilitumia kwa ufasaha utaondokana kabisa na tatizo hilo.  Pia inasaidia kuondoa mafuta tumboni na kupunguza uzito wa mwili.
Nimesema papai jekundu kwa kuwa yapo pia yenye rangi ya njano ndani.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment