Saturday, 26 May 2018

Penda kula uyoga ni kinga na tiba ya magonjwa mengi


Uyoga

UYOGA ni mboga inayoliwa na wanajamii wengi. Mboga hii ni kama nyingine za majani ambazo ni mchicha, chaina na sukumawiki.

Uyoga umegawanyika katika makundi mawili ambayo ni ule wa kupandwa na unaoota wenyewe porini.

Wataalamu wa tiba na lishe wanasema sasa uyoga utumiwe kama mboga za majani ukiwa mbichi au mkavu.

Wanajamii wanaweza kuandaa uyoga (mboga) mbichi au mkavu baada ya kuanikwa na kutunzwa vizuri.

Magonjwa ya tezi la shingo, kiharusi, maumivu ya viungo, kurefusha maisha kwa waathirika na magonjwa ya ngozi yanaweza kukingwa na kutibiwa kwa uyoga.

Miongoni mwa dawa za kisasa nyingi zimeandaliwa kwa uyoga. Mwaka 1928, tabibu wa Uingereza, Alexander Fleng aligundua dawa ya antibiotic inayojulikana kama penincillin ambayo ni nzuri hadi sasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuua bakteria.

Pia dawa nyingine cyclosporin A inayofanya kazi ya kukinga mwili ambayo hutumiwa katika upandikizaji viungo kama ini, figo, moyo na mifupa zote hizi zimetokana na uyoga.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment