Sunday, 6 May 2018

Rais Dk. John Magufuli akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali katika ziara yake mkoani Morogoro ambako pia alifungua daraja la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika Mto Kilombero

Rais Dk. John Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula Kona, wilaya ya Kilombero wakati akiwa njiani kuelekea kufungua daraja kubwa la Mgufuli linalopita katika Mto Kilombero lenye urefu wa mita 384.

Rais Dk. John Magufuli akimpongeza mwanafunzi wa shule ya sekondari Mang’ula, Mrindoko Msangi baada ya kumkabidhi sh. milioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo. Mwanafunzi huyo alimweleza Rais Magufuli kwa ufasaha kero inayowakabili shuleni hapo.


Rais Dk. John Magufuli akizungumza na wananchi wa Kiberege wakati akiwa njiani kuelekea kufungua daraja la Magufuli linalopita katika Mto Kilombero katika wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.


Rais Dk. John Magufuli na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa daraja la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika Mto Kilombero, mkoani Morogoro.


Rais Dk. John Magufuli akipeana mkono na mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali mara baada ya kufungua daraja la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika Mto Kilombero mkoani Morogoro.

Rais Dk. John Magufuli akifurahia jambo na mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali baada ya kufungua daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika Mto Kilombero mkoani Morogoro.


Rais Dk. John Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, mkewe Mama Janeth Magufuli, viongozi mbalimbali wa dini, Serikali, wabunge wa mkoa wa Morogoro na  viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika Mto Kilombero, mkoani Morogoro.

Rais Dk. John Magufuli akizungumza katika msiba wa wanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerald mara baada ya kutoa rambirambi wakati akiwa njiani kuelekea kufungua daraja la Mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lilinalounganisha wilaya ya Ifakara na Malinyi mkoani Morogoro.


Rais Dk. John Magufuli akitoka kwenye msiba  wa mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerald mara baada ya kutoa rambirambi wakati akiwa njiani kuelekea kufungua daraja la Kilombero (Daraja la Magufuli).(PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment