Sunday, 6 May 2018

Rais wa Iran aitabiria majuto Marekani ikisitisha makubaliano ya nyuklia


Rais wa Marekani, Donald Trump (kushoto) na wa Iran Hassan Rouhani.

RAIS wa Iran, Hassan Rouhani, amesema endapo rais Trump atafanikiwa kusitisha makubaliano ya mpango wa nuklia na Tehran, Marekani itambue wazi itakabiliwa na "majuto ya kihistoria".
Tamko hilo la Rais Rouhani, lililotolewa kwenye runinga, limekuja wakati waziri wa masuala wa nchi za nje wa Uingereza, Boris Johnson, amekwenda mjini Washington kama sehemu ya jitihada za kumshawishi Rais Trump na utawala wake wasiutelekeze mpango wa nyuklia.
Tarehe ya mwisho ya kutoa uamuzi kwa serikali ya Marekani kuhusu Iran inatarajiwa kufikia ukingoni wiki moja ijayo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema rais wa nchi hiyo amesisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kwamba Iran haipati kamwe silaha ya nyuklia.
Katika siku za hivi karibuni, Rais Trump alimweleza rais wa Ufaransa aliyekuwa ziarani na viongozi wa Ujerumani kwamba ana amini makubaliano ya kimataifa ya kukabiliana na mpango wa nyuklia wa Iran ulikuwa mzuri sana.
Wakati wote Korea Kaskazini imekuwa ikiikosoa Marekani lakini kumekuwa na mashambulizi machache katika wiki za hivi karibuni, wakati wa mipango ya Rais Trump kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un ikiendelea.
Taarifa hii ya karibuni ni kama tahadhari ya kuwa majadiliano kati ya nchi hizo mbili hayatakuwa rahisi.
Wakati huo huo Korea Kaskazini imeishutumu Marekani kwa uchochezi wa makusudi dhidi ya Pyongyang kwa kutoa ushauri wa vikwazo havitaondolewa hadi hapo itakapondoa silaha zake za nyuklia.

No comments:

Post a Comment