Saturday, 5 May 2018

Serikali kuajiri madaktari 3000


Rais Dk. John Magufuli

Claudia Kayombo

SERIKALI inakusudia kuajiri madaktari 3,000 katika kipindi cha mwaka huu ili kuondokana na changamoto ya uhaba wa wataalam wa afya kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana na Rais Dk. John Magufuli katika ziara yake kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro.

Amesema anatambua changamoto wanazokumbana nazo wananchi hususan maskini hivyo uhakika wa huduma za afya utasaidia jamii kubwa ya watanzania kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya.

Hali kadhalika ameahidi kuondoa tatizo la maji katika vijiji vingi vya mkoa huo. Amewataka wananchi wa mkoa wa Morogoro kulima mazao mbalimbali ili taifa lisipungukiwe chakula.

Aidha, katika ziara hiyo Rais Magufuli katika maeneo yote aliyozungumza na wananchi hakuacha kusisitiza umuhimu wa kulinda amani ya nchi iliyopo.

No comments:

Post a Comment