Tuesday, 8 May 2018

Serikali kupunguza tatizo la watumishi, vifaa tiba nchini


Josephat Kandege

Mary Meshack, Dodoma

SERIKALI imesema itaendelea kuhakikisha hospitali, vituo vya afya na zahanati zinapatiwa vifaa tiba na watumishi wa afya katika maeneo mbalimbali nchini.

Naibu wa Waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Newala Vijiji, Rashidi Akbar.

Katika swali lake la msingi mbunge aliihoji serikali ina mpango gani wa kuipatia hospitali ya wilaya ya Newala watumishi na vifaa tiba.

Kandege amesema hospitali hiyo imeomba ipatiwe wahudumu wa afya 60 na kwamba miongoni mwa wafanyakazi 59,000 ambao serikali inatarajiwa kuwaajiri siku za hivi karibuni ni wa kada ya afya na elimu.

Hivyo punde watumishi hao watakapoajiriwa hospitali na Newala na nyingine nchini zitapatiwa wafanyakazi. Kandege alikiri kuwepo uhaba wa wafanyakazi wa afya katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment