Monday, 7 May 2018

Shamba la mfano la eka 300 lalimwa na chuo kikuu Sokoine


Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako

Claudia Kayombo

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine mwaka huu kimelima shamba la mfano lenye ukubwa wa eka 300.

Pia kimepanda miche 4,000 ya mipapai inayokomaa kwa muda wa miezi mitano kutokana na mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na chuo hicho.

Prof. Ndalichako ametoa kauli hiyo leo Mei 7, 2018  mbele ya Rais Dk. John Magufuli aliyetembelea chuoni hapo ambapo pamoja na mambo mengine alipokea kero mbalimbali na kuzitolea majibu kutoka kwa wanafunzi, wahadhiri na wafanyakazi wa kada nyingine.

Aidha, waziri huyo amesema pamoja na jitihada hizo nzuri pia ameagiza uongozi wa shule hiyo kuwa na ‘green house’ ili chuo hicho kiwe darasa la mfano kwa yeyote anayekitembelea ili kujifunza masuala ya kilimo na ufugaji.

Prof. huyo amesema anaweka mkazo huo kwa kuwa Sokoine ni chuo pekee nchini kinachotoa mafunzo ya kilimo na ufugaji ndiyo maana hata katika bajeti kimetengewa kiasi kikubwa cha fedha ikilinganishwa na vyuo vikuu vingine.

No comments:

Post a Comment