Sunday, 20 May 2018

Shina la mgomba msaada kwa mgonjwa asiye na tumaini la kuishi


 
                    Shina la mgomba

ZAO la mgomba ni maarufu katika mikoa mingi hapa nchini licha ya kuwa ustawishaji wake unatofauti baina ya mkoa mmoja na mwingine.


Mgomba unastawi katika eneo lenye ardhi yenye rutuba, maji ya wastani na hali ya hewa yenye ubaridi.

Licha ya zao hilo kuwa maarufu karibu kila mkoa kutokana na historia yake, mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Manyara, Mara, Tanga, Morogoro, Kigoma na Pwani inastawisha kwa wingi zaidi.

Mikoa ya Kagera, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Manyara, ndizi ni chakula kikuu, huku maeneo mengine zao la mgomba likistawishwa kwa ajili ya biashara.

Migomba inaweza kupandwa katika misimu yote ya mwaka kwa kuwa zao hilo linastahimili ukame. Asili ya mgomba ni Malaysia na India nchi zilizoko Kusini Mashariki mwa Asia.  

Hata hivyo, wakati jamii kubwa ikitumia ndizi kama chakula kikuu, au matunda, shina la mgomba lina maajabu makubwa katika tiba.

Shina hilo ambalo lipo mithiri ya kiazi, likikaushwa unga na wake ukiwekwa katika uji mwepesi na kupewa mgonjwa mwenye hali mbaya ambaye hawezi kuinuka na yule ambaye maradhi anayougua hayajulikani inasaidia sana.

Dawa hii ina nguvu ya kutibu maradhi hayo kwa sababu kiasili mgomba unahimili changamoto nyingi ikiwemo jua na hali nyingine ambayo mimea mingine haiwezi.

Mgomba pia huzikwa badala ya mtu katika kaburi ambalo limeshindikana kuzikwa mfu kutokana na sababu mbalimbali, pia mtoto anayezaliwa kabla ya wakati huzikwa katika migomba hali inayoonesha kuwepo uhusiano baina ya mwanadamu na mmea huo.

Mchanganua huu kwa ufupi umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au nipigie simu kwa namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment