Saturday, 5 May 2018

Spika Job Ndugai akutana na kuzungumza na msafara wa Mchungaji na Mwalimu Christopher Mwakasege na mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini, John Shibuda ofisini kwake mjini Dodoma


Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kiongozi wa msafara wa Mwalimu na Mchungaji Christopher Mwakasege (katikati) ambaye pia anatoa huduma ya Mana pamoja na mke wake, Daina Mwakasege (wa pili kulia) walipomtembelea jana Mei 4, 2018, ofisini kwake mjini Dodoma.

Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mwalimu Mchungaji Christopher Mwakasege (kulia) alipomtembelea jana Mei 4, 2018, ofisini kwake mjini Dodoma.


Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Diana Mwakasege (kulia) ambaye ni mke wa Mwalimu Mchungaji Christopher Mwakasege walipomtembelea jana Mei 4, 2018 Ofisini kwake mjini Dodoma. Katikati ni Mwalimu Mchungaji Christopher Mwakasege.


Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Anna Lupembe (aliyesimama) pale ugeni ulioongozwa na Mwalimu na Mchungaji Christopher Mwakasege (wa tatu kulia) aliyeambatana na mke wake, Daina Mwakasege (wa pili kulia) walipomtembelea jana Mei 4, 2018, ofisini kwake mjini Dodoma.


Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda (kulia) alipomtembelea jana Mei 4, 2018 ofisini kwake mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments:

Post a Comment