Monday, 21 May 2018

Sugu apokelewa kwa shangwe bungeniMbunge Joseph Mbilinyi 'Sugu' alivyoingia bungeni leo asubuhi (PICHA NA GAZETI LA MWANANCHI ) 

Mary Meshack, Dodoma

MBUNGE wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo ameingia kwa mara ya kwanza bungeni tangu atoke gerezani.

Alikuwa anatumikia adhabu ya kifungo gerezani mwezi Februari mwaka huu baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la  kumfedhehesha Rais Dk. John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, jijini Mbeya.

Hata hivyo, baada ya kuingia bungeni, wabunge wenzake hususan wa upinzani walilipuka kwa shangwe huku wengi wakitaka kupeana naye mikono kama ishara ya kumtakia heri na kumkaribisha.

Alikuwa akitumia adhabu hiyo ya kifungo cha miezi mitano kwenye gereza la Ruanda, mkoani Mbeya, alikopelekwa baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa hilo.

Wakati wabunge hao wakishangilia, Mwenyekiti wa Bunge, aliyekuwa akiongoza kikao hicho cha 33, cha mkutano wa 11, leo Mei 21, 2018, Andrew Chenge,  aliwaomba wamalize shangwe hizo ili waweze kuendelea na kipindi cha maswali na majibu.

No comments:

Post a Comment