Wednesday, 9 May 2018

Tanzania yatajwa kuwa ndiyo chimbuko la mwanadamu wa kale duniani


Japhet Hasunga


UTATA uliokuwa ukiendelea duniani kuwa mwanadamu wa kwanza alitokea wapi umemalizia baada ya jopo la wataalam kubaini kuwa alitokea barani Afrika, nchini Tanzania.

Jopo hilo lililoundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii libaini hilo baada ya ushahidi wa vinasaba kuonesha kuwa alitokea Bonde la Olduvai.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amebainisha hilo wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya ufugaji nyuki alioutisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo, jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Amesema  utafiti huo umeshirikisha wataalamu kutoka mataifa mbalimbali duniani na kuwa kumalizika kwake kutaiwezesha sekta ya utalii nchini kukua kwa kasi sanjari na kuongezeka kwa pato la taifa.

No comments:

Post a Comment