Saturday, 5 May 2018

Tatizo la maji Mikumi Profesa Jay amwangukia Magufuli


Joseph Mbilinyi

Claudia Kayombo

MBUNGE wa Mikumi, Joseph Mbilinyi ‘Profesa Jay’ (Chadema), amemwomba Rais John Magufuli kumaliza tatizo kubwa la maji katika jimbo lake.
Amesema tathmini imefanyika na kwamba zinatakiwa sh. bilioni mbili kumaliza tatizo hilo.

Alitoa kauli hiyo jana wakati wabunge walipopewa fursa ya kuwasalimia wananchi katika ziara ya Rais Mafuguli inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Morogoro.

Mbunge Mbilinyi ambaye pia ni mwanamuziki amesema zipo changamoto nyingi katika jimbo lake, lakini tatizo la maji ni kubwa zaidi.

Pia amemwomba Rais Magufuli kuwezesha waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha sukari kupata malipo yao ambayo wanayadai kwa muda mrefu huku wengine wakipoteza maisha yao huku wakingali hawajapewa fedha zao.

No comments:

Post a Comment