Wednesday, 30 May 2018

Tumia bidhaa asili kukinga mwili dhidi ya magonjwa


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akiwa ameshika ndizi mbivu ambazo zinatumika kuandaa virutubisho vinavyoongeza kinga ya mwili.


ZIPO sababu nyingi zinazochangia kinga ya mwili wa binadamu kushuka, miongoni mwazo ni ulaji wa lishe duni. Mtu anapokumbwa na tatizo la kushuka kinga za mwili anakuwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa mbalimbali.

Hata hivyo, baadhi ya watu unapozungumzia suala la kinga za mwili kushuka mawazo yao yanawapeleka katika ugonjwa wa Ukimwi. Kushuka kinga za mwili kunasabisha maradhi mengi kikiwemo Kifua Kikuu (TB), na mkanda wa jeshi.

TB na mkanda wa jeshi ni maradhi ambayo yalikuwepo miaka mingi kabla ya kugunduliwa Ukimwi. Wakati huo wazee wetu walitumia bidhaa asili kuchochea ongezeko la kinga za mwili.

Leo ninawaletea bidhaa hizo ambapo ukitumia kulingana na maelekezo utabaini mabadiiko makubwa katika mwili wako au wa ndugu yako anayekabiliwa na upungufu huo.

Chukua ndizi mbivu tatu, parachichi tatu, mayai matatu ya kuku wa asili, maziwa freshi nusu lita, na asali vijiko vikubwa vitatu. Changanya mchanganyiko huo kisha kunywa glasi moja asubuhi na nyingine jioni utaona mabadiliko makubwa katika mwili wako.

Mchanganyiko huo utamkinga mtumiaji dhidi ya magonjwa mbalimbali lakini pia utaiacha katika nuru ngozi iliyokuwa imeshambuliwa na upele au majipu.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment