Wednesday, 2 May 2018

Tumia kokwa la embe kumaliza tatizo la kutokwa maji meupe ukeni


Kokwa la embe

MWILI wa mwanamke unapolemewa na sumu za aina mbalimbali zinazotokana na chakula na vinywaji, husababisha sumu hizo kushindwa kutokea kwenye njia za kawaida za jasho, mkojo, choo na hewa wakati wa kupumua.

Mwili huanzisha njia nyingine za kutoa uchafu kupitia kwenye utando wa mfuko wa uzazi na kwenye uke kama maji maji meupe.

Hali hiyo si ya kawaida, ikishatokea inaweza kuendelea kwa muda wa majuma kadhaa, hata miezi na kama haijadhibitiwa kwa tiba, inakuwa ya kudumu na kuleta udhia.

Mara nyingi tatizo hilo huambatana na maumivu ya mgongo, mashavu ya miguu na tumbo.

Zipo aina mbalimbali za tiba asili ambazo zinaweza kumsaidia mwathiriwa kuondokana na tatizo hilo ambazo ni pamoja na mbegu za embe, mpera, muarobaini, bamia, mchicha na hina.

Mbegu ya embe

Mbegu ya embe iponde na kuwa ujiuji,chukua kijiko cha chai cha ujuuji huo, weka sehemu ya uzazi asubuhi na jioni, endelea kufanya hivyo kwa muda wa wiki tatu. Nusu kijiko cha chai cha unga wa mbegu za embe zilizokaushwa katika kivuli unaweza kutumia pia badala ya ujiuji.

Mpera

Nusu kilo ya majani ya mpera, chemsha katika lita mbili za maji kwa muda wa dakika 20. Baada ya maji kupoa, tumia maji hayo kuoshea sehemu za uzazi mara tatu kwa siku muda wa siku 21.

Muarobaini

Majani ya muarobaini nusu kilo ongeza lita mbili za maji chemsha kwa muda wa dakika 15, baada ya kupoa tumia kuoshea sehemu za uzazi kutwa mara mbili kwa muda wa siku 21.

Bamia

Nusu kilo ya bamia, kata vipande na chemsha katika lita moja ya maji kwa muda wa dakika 20, baada ya kupoa kunywa nusu glasi mara sita kutwa kwa muda wa siku 10.

Mchicha

Mizizi ya mchicha nusu kilo, ioshe ndani ya maji safi, iponde na loweka ndani ya lita moja ya maji kwa muda wa saa moja, kunywa glasi moja ya maji hayo asubuhi na jioni kwa muda wa siku 14.

Hina

Ponda majani ya hina hadi yawe kama ujiuji, chukua kijiko kimoja cha chai cha uji huo weka sehemu za uzazi asubuhi na jioni kwa muda wa siku 14.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment