Tuesday, 29 May 2018

Tumia majani ya mstafeli na mtopetope kujikinga sarataniSehemu ya mti wa mstafeli yenye majani na tunda.

SARATANI ni ugonjwa mkubwa na hatari, usipoanza matibabu mapema unaweza kupoteza maisha.

Zipo aina mbalimbali za maradhi ya saratani, ambapo leo nimelenga kuwaeleza namna ya kujikinga nayo.

Mungu ametuumbia mimea ya aina mbalimbali ili iwe msaada kwetu katika suala zima la tiba ya magonjwa mbalimbali yanayotusumbua katika jamii.

Hakuumba ugonjwa wowote bila dawa. Alianza kuumba dawa kwanza kisha akaleta maradhi, hiyo hata katika vitabu vyetu vitakatifu Quran na biblia vimebainisha.

Kama ilivyo njaa inapomkabili mtu anapaswa kula chakula kwa wakati ndivyo magonjwa nayo yanahitaji tiba ya mapema, ukichelewa inakuwa shida.

Katika kujikinga na saratani za aina mbalimbali, tumia majani ya mstafeli na mtopetope yanafaa sana, tuyatumie mara nyingi tuwezavyo.

Kausha kwenye kivuli majani haya kisha saga, unga wake tumia katika maji moto au uji mwepesi.

Sehemu ya mti wa topetope pori yenye majani na matopetope yaliyowiva.

Tumia dawa hii kujikinga maradhi haya na mengine nyemelezi na sugu kila mwaka japo kipindi cha miezi miwili.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment