Tuesday, 22 May 2018

Tumia mchanganyiko huu kuondokana na figo, kiharusi

Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia jinsi  mchanganyiko wa viungo ulivyo tiba mujarabu wa maradhi mbalimbali.

TANGAWIZI, bizari na mdalasini ni viungo muhimu kwa mapishi ya kila siku katika jamii zetu. Viungo hivyo vinajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kunosha vyakula.

Hata hivyo, tangawizi ikichanganywa na bizari, kungumanga, mdalasini na alikisusi inakuwa dawa mujarabu kwa tiba ya maradhi mengi na si tu viungo pekee kama tulivyoona awali.

Mchanganyiko huo unasaidia kutibu mapafu, kuondoa mawe kwenye figo, kuongeza afya ya akili, kumwongezea nguvu mgonjwa aliyekumbwa na kiharusi, maradhi ya athma, kupunguza uzito wa kupita kawaida na matatizo ya kubana mbavu.

Unatakiwa kutumia mchanganyiko huu wa unga kwenye maji moto, kuchanganya na asali au na maziwa freshi.

Mchanganua huu kwa ufupi umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au endelea kutembelea tovuti yetu www.dkmandai. com ili kujifunza mambo mbalimbali ya kiafya.

No comments:

Post a Comment