Saturday, 5 May 2018

Tumia mkojo ni tiba ya mdudu wa kidole


Namna unavyoweza kuhifadhi mkojo kwa ajili ya kutibu mdudu wa kidole.


MDUDU wa kidole ni aina ya jipu kwenye ncha ya kidole cha mkononi hasa chini ya ukucha. Ugonjwa huu kwa kawaida huitwa ‘mdudu’.

Tatizo hilo linaweza kusababisha maumivu makali na kuleta usumbufu wa muda mrefu. Linaweza kutibiwa kwa maziwa, ndimu, unga wa ngano, kitunguu maji na mkojo.

Kitunguu maji/mkojo

Kama tatizo la ugonjwa ndiyo linaanza linaweza kudhibitiwa lisiendelee kwa kutumia mkojo. Kinga mkojo katika chupa au chombo ambacho kidole kinaweza kuingia, ingiza kidole katika mkojo mara kwa mara.

Au ponda kitunguu maji, ongeza maji kidogo ili kupata mchanganyiko  uliokolea, chovya kidole mara kwa mara ndani ya mchanganyiko huo.

Maziwa

Mililita 100 za maziwa yasiyoondolewa mafuta, changanya na mafuta ya nyonyo matone 10, funga katika kidole eneo lililoathirika kwa kitambaa safi kilicholowanishwa  na mchanganyiko huo.

Kitambaa kinapokaribia kukauka, lowanisha tena kwa mchanganyiko huo kwa wakati wote wa mchana. Tiba hii ni ya siku tatu hadi tano.

Ndimu

Toboa ndimu upande mmoja ukubwa wa kidole kilichoathirika,  Ingiza kidole katika shimo la ndimu, badilisha ndimu kila siku hadi kidole kitakapopona. Tiba hii endelea nayo siku tatu hadi tano.

Unga wa ngano

Chukua unga wa ngano kidogo, changanya na maji hadi uonekane kama tui la nazi, ongeza sukari kidogo na matone 15 ya mafuta ya nyonyo, koroga kisha pasha moto mchanganyiko huo na upake kwa wingi katika kitambaa kisafi, funga katika kidole kilichoathirika, fanya tiba hii  kutwa mara mbili (asubuhi na jioni) kwa muda wa siku tano.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia virutubisho tiba vinavyozalishwa na kampuni yetu malidhawa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment