Sunday, 6 May 2018

Tumia ndula unapong’atwa na mbwa mbali na kituo cha afya


Ndula

BAADA ya kung’atwa na mbwa asiye na chanjo, osha kwa sabuni sehemu iliyoathirika kwa muda wa dakika tano au zaidi, toa masalia yote ya uchafu katika eneo husika. Muathirika ni vema akimbizwe hospitaliau katika kituo cha chanjo haraka.

Kwa aliye mbali na huduma hizo kwa maana ya kuwa yupo porini sana au vijiji vya mbali au popote na akang’atwa na mbwa, mbweha, paka au jamii nyingine ya wanyama hao, aoshe kidonda huku akiwa amefunga kitambaa kwa juu kidogo kutoka sehemu yenye jeraha.

Baada ya hapo chukua tunda la ndula lililowiva au bichi pasua katikati na usugue sana sehemu hiyo yenye jeraha. Vumilia ukilisugua hapo utaona damu nyeusi ikitoka, hiyo yote ni sumu.

Endelea kusugua hadi uone damu nyekundu inatoka, ndipo sumu itakuwa imekwisha. Tengeneza bandeji yenye dawa hii, ondoa na kuosha kila baada ya saa nne na kubandika nyingine .

Ikiwa umeng’atwa na mbwa au paka ambao wanaonekana kuwa na afya nzuri  maana ya kuwa hawana maradhi basi mgonjwa atatazamwa ndani ya siku 10.

Kama haitaonekana dalili ya kichaa cha mbwa basi haina haja kupewa matibabu zaidi, ila kama umeng’atwa na wanyama wa porini basi ni vema upewe chanjo na uzingatie matumizi yake.

Ikumbukwe kuwa ugonjwa huu haupatikani kwa kung’atwa na nyoka ila wanyama wenye damu moto.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu+255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment