Saturday, 5 May 2018

Ugoro, tumbaku husaidia kuzuia damu kutoka


Ugoro

ZIPO tiba nyingi wanazitumia matabibu kuwaganga watu (mtu) wanapotokwa damu baada kujeruhiwa.

Dawa hizo ni pamoja na utando wa buibui, maji baridi na jivu, ugoro na tumbaku, mkaa, bizari na chokaa, bizari na chumvi, embe, muarobaini na mpungate.

Ugoro na tumbaku

Baada ya kuumia, safisha kidonda, nyunyizia ugoro au tumbaku, nikotini iliyomo kwenye tumbaku huifinya mishipa isitoe damu.

Utando wa buibui

Baada ya kujikata au kuumia kama kidonda siyo kikubwa sana, kioshe kwa maji ya chumvi halafu weka utando wa buibui. Utando huo una dawa inayoitwa akinidini ambayo inasaidia sana kugandisha damu.

Maji baridi na jivu

Kitambaa safi kiweke ndani ya maji baridi kisha kitoe kisha kanda katika jeraha, kama damu inaendelea kutoka, chukua jivu la pamba au kitambaa hariri weka kwenye jeraha. Jivu la kuni au mkaa pia bandike katika kidonda linasaidia pia.

Chokaa

Weka chokaa katika kidonda kuzuia kuvuja damu, baada ya hapo kunywa glasi moja au mbili za maji baridi.

Mkaa

Osha kidonda kwa maji yenye chumvi, nyunyizia unga wa mkaa katika sehemu ya jeraha, kunywa glasi moja au mbili za maji baridi

Bizari na chokaa

Changanya bizari iliyopondwa na unga wa chokaa, weka sehemu yote ya jeraha damu itaacha kutoka.

Bizari na chumvi

Changanya bizari na chumvi, weka kwenye jeraha itazuia damu kuendelea kutoka.

Embe

Mbegu ya embe, majani ya mwembe au gome lake, choma mojawapo ili kupata majivu, weka kwenye jeraha linalovuja damu, itakoma kutoka.

Muarobaini

Ponda majani ya muarobaini bandika kwenye jeraha.

Mpungate

Ikiwa umekosa maji safi ya kusafishia kidonda safisha kidonda kwa kutumia utomvu wa mpungate.

Kata kipande cha mpungate, funga kwenye jeraha, baada ya saa tatu ondoa safisha kidonda kwa sabuni na maji yaliyochemshwa.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment