Thursday, 17 May 2018

Ujue mlangamia mmea wa ajabu unaokua bila mizizi ni kinga na tiba


Mlangamia unavyotambaa juu ya miti

MLANGAMIA ni jina la mmea wa ajabu unaokua bila mizizi. Mmea huu asili si maarufu sana miongoni mwa wanajamii bali kwa matabibu wa tiba asili wenye ujuzi.

Wengi wao wanautumia kutibu maradhi mbalimbali yanayozikumba jamii nyingi siku hizi yakiwemo yanayoshindikana katika tiba za kisasa. Ni mmea wa ajabu kwa kuwa una mzizi usioonwa na wengi bali na baadhi tu ya matabibu walio na ujuzi wa tiba hii.

Mmea huu unaotambaa juu ya miti unapokuwa mchanga unachomoza kutoka katika mzizi huo wa ajabu unapoanza kutambaa unakatika na kuendelea kutambaa wenyewe. Hata hivyo, iwapo tabibu akaja kuchimba mzizi wake ulio kama kiazi, unakauka.

Una mafanikio makubwa katika tiba hususan kwa wanaosumbuliwa na maradhi ya kifadulo, athma, kukatika sauti na ni kinga nzuri dhidi ya nguvu za giza.

Mzizi wa mmea huu huwekwa katika nyumba ni kinga nzuri dhidi ya nguvu za giza pia ngariba wanauweka kwenye nyumba wanayowawekwa vijana waliotahiriwa na kwamba mtu mbaya (mchawi) anapokwenda eneo hilo haoni chochote.

Mchanganua huu umeletwa kwako na mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana na mtaalam Mandai kwa simu namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment