Saturday, 12 May 2018

Ujue mpangaa mti unaoota juu ya mwingine wenye maajabu katika tiba


 
Unaweza kuukuta mpangaa kwenye miti mikubwa kama huu

MPANGAA ni mti unaoota juu ya mti mwingine mkubwa uliodumu kwa muda mrefu. Mti huo ni lazima uwe ni ule uliopambana na jua, mvua na radi katika misimu mbalimbali ya vipindi vya miaka kadhaa.

Tangu wakati wa mababu zetu, mti huu umetumika kutibu magonjwa mengi ambayo yameshindwa kuonekana katika vipimo vya kisasa na mikwamo ya kimaisha.

Matumizi

Twanga majani ya pangaa mwogeshe mtoto wakati wa asubuhi ataondokana na homa zinazomkumba mara kwa mara. Pia mti huu unasaidia maradhi ya degedege kwa watoto.

Kijiko kimoja cha unga wa majani ya pangaa weka katika uji mwepesi ulio katika kikombe cha chai mpe mwanamke mwenye tatizo la kupevusha mayai atumie kutwa mara mbili kwa hata wa mwezi mmoja ataondokana na tatizo hilo.

Uji huo pia unasaidia kwa kina mama wenye uvimbe katika via vya uzazi na hata wale wanaoshindwa kupata watoto kutokana na nguvu za giza.

Kama nilivyosema mmea huu una uwezo mkubwa na unaaminiwa tangu enzi za mababu zetu.Narudia tena kuwa dawa hii inasaidia sana hususan kwa magonjwa yaliyoshindikana hospitalini.

Kwa mwenye tatizo asisite kuja makao yetu makuu ambapo utapata maelezo ya kina ya namna sahihi ya kutumia mmea huu kuondokana matatizo mbalimbali.

Mchanganuo huu umeletwa kwako nami Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho tiba vyetu.

No comments:

Post a Comment