Saturday, 19 May 2018

Unazijua faida za maji ya bahari? Hizi hapa


Makundi ya watu wakiogelea katika ufukwe wa bahari ya Hindi, eneo la Cocobeach, Dar es Salaam. Wakati wa sikukuu watu wengi zaidi hukusanyika maeneo hayo.

WATU wengi wanaopenda kwenda baharini kuoga au kuota jua wanafurahi kuwepo eneo hilo, sina uhakika iwapo wote wanatambua faida za kuoga au kuwepo katika fukwe mbalimbali za bahari.

Kimsingi maji ya bahari yana msaada mkubwa kwa maisha ya binadamu, hata wenzetu wazungu pia wanapenda sana kuwepo maeneo hayo, bila shaka nao wanatambua faida zake.

Kizibo kimoja cha chupa ya soda chenye maji ya bahari changanya na lita moja yasiyo ya bahari, kunywa, yanaondoa tatizo la maradhi ya mifupa, penda kufanya hivyo mara kwa mara.

Katika kipindi cha mwisho au mwanzo wa mwaka maeneo mbalimbali ya fukwe za bahari duniani yanafurika watu, wengi wao wanaoga kwa kuamini kuwa wanaondoa mikosi.

Matabibu wengi wa tiba asili zamani hadi sasa wanatumia maji ya bahari kutibu magonjwa mbalimbali, pamoja nao walimu wanawaosha wagonjwa wao maji ya bahari kuwaondolea magonjwa mbalimbali.

Hata taka za baharini nazo zinatumika na matabibu hao kutibu wagonjwa wao magonjwa mbalimbali.

Maji hayo yanaaminika kwa kuwa yanapita katika mabara mengi hivyo tiba yake ni nzuri.

Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au nipigie simu kwa namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment