Friday, 18 May 2018

Vikanga, vikango visipotibiwa vinaweza kuua wenza au watoto


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumza jambo akiwa makuu ya ofisi yake Ukonga, Mongo la ndege, Dar es Salaam.

JANA nilieleza iwapo umepatwa na tatizo la vikanga kwa mwanamke na vikango kwa mwanaume unaweza kutibiwa tatizo hilo kwa tunda za tunguja (tula) ambapo utazichemsha kisha kujifusha sehemu za uzazi au haja kubwa.

Sikueleza madhara anayoweza kupata mtu mwenye tatizo hilo iwapo hatapata matibabu stahiki.

Tangu zamani maradhi haya yalikuwa yakiwakumba wanajamii na mababu zetu walikuwa wakiwatibu na kuwanusuru na athari zake ambazo ni mbaya kwao na jamii.

Wote mwanamke na mwanaume wenye tatizo hilo wanaweza kuondokewa na wapenzi wao, watoto, kutofanikiwa katika harakati mbalimbali za kujikwamua kimaisha, kukataliwa na kunenewa vibaya na wanajamii bila kosa lolote.

Chanzo cha vikanga na vikango linaweza kuwa ni tatizo linalosababishwa na watu dhidi ya wenzao wanaowaonea kijicho, lakini pia huota vyenyewe na vyote kwa pamoja vinatibiwa kwa tiba hii.

Ninapozungumzia habari za watu kuwasababishia wenzao tatizo hili (kuwaloga) baadhi yetu tunaweza kupata picha moja kwa moja kuwa mimi ni mshirikina, vyoyote utakavyofikiri kuhusu hili lakini ukweli unabaki kuwa hivyo.

Mambo ya nguvu za giza tunayoyazungumza leo yapo hata ndani ya  vitabu vitakatifu, kukaa kimya hakumaanishi kuwa ni njia ya kukwepa jambo hili.

Hata hivyo, kwa kuwa maradhi haya ni ya siri wapo watu ambao hawajitokezi hadharani kuyazungumzia na hivyo athari zake kuendelea kuwaathiri.

Ukweli ni kwamba kama una tatizo hilo fika leo makao yetu makuu Ukonga, Mongo la ndege, Dar es Salaam na tatizo hilo utaondokana nalo.

Vikanga na vikango ni nini?

Mtunguja (mti wa tunguja) ni mmea unaofanana na mnyanyachungu, ikiota pamoja shambani ni vigumu kuitofautisha.

Unasaidia kupambana na maradhi mbalimbali ikiwemo  vikanga, vikango, bawasili, kichwa, kizunguzungu na ngili.

Kwa anayesumbuliwa na vikanga (vipele vinavyoota kuzunguka sehemu ya haja ndogo ya mwanamke) na vikango (vipele vinavyoota sehemu ya haja kubwa ya mwanaume) chukua matunda ya tunguja weka katika sufuria au chungu funika vizuri kuzuia mvuke baada ya kuweka maji yachemshe.

Baada ya kuipua, chukua meza ilaze upande mmoja juu ya dawa hii kisha kaa ukiwa hujavaa nguo ya ndani ili mvuke uingie katika sehemu ya haja kubwa au ndogo ikiwa unakabiliwa na matatizo hayo.

Wakati huo uwe umejifunika kwa nguo nzito. Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili. Kama huna stuli toboa kiti cha kukalia jikoni kisha kiweke juu ya dawa baada ya kuifunua kaa hapo ili mvuke ukuingie kupitia tundu hilo.

Mizizi ya tunguja pia inasaidia kupambana na maradhi ya ngili, hivyo ichukue kiasi cha kujaa mkono, ioshe vizuri kisha ichemshe na kunywa maji yake.

Majani ya tunguja pia yanasaidia tatizo la kipanda uso, yachemshe na kisha jifushe kama nyungu yanasaidia kuondoa kipanda uso na homa za mara kwa mara.

Mtunguja

Ukiponda majani yake na kupata unga utumie katika maji moto au uji mwepesi, unasaidia kwa wenye tatizo la kutapika na kuharisha.
Mchanganua huu umeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment