Tuesday, 29 May 2018

Wajua kinyesi cha tembo kinamaliza kipanda uso?


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia namna kinyesi cha tembo kinavyoweza kua suluhisho la tatizo la kipanda uso na kizunguzungu.


KIZUNGUZUNGU na kipanda uso ni tatizo linalowasumbua watu wengi. Kitaalamu tatizo hilo linasababishwa na mzunguko hafifu wa damu.

Mara nyingi baadhi ya watu wanapokumbwa na tatizo hilo wanaingiwa na dhana kuwa wamevamiwa na majini au pepo wachafu.

Ni kweli majini na mapepo wapo ambao wakati mwingine wanaweza kusababisha tatizo hili, lakini binafsi naamini ukitumia mavi ya tembo yana uwezo mkubwa wa kulikabili.

Chukua mavi ya tembo choma kisha jifukize moshi wake, unaondoa tatizo la kipandauso na kizunguzungu.

Pia tatizo la kutokwa damu puani, limekuwa likiwatatiza baadhi ya watu, jifukize mavi haya ya tembo asubuhi na jioni.

Mavi ya tembo pia ukichoma ndani ya nyumba yenye mauza uza yataondoa tatizo hilo. Tunayaamini mavi ya tembo kwa kuwa ana kula mimea mingi ya aina mbalimbali.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment