Monday, 28 May 2018

Wajua limau ni kiboko ya fangasi kandida?

Limau

KINAMAMA wengi baada ya kujisaidia haja ndogo, hujisafisha kwa maji namna wanayoijua wao. Miongoni mwao wanakuwa makini kujifuta baada ya kujisafisha ili kubaki wakavu.

Wale wanaoshindwa kufanya hivyo mara nyingi wanakabiliwa na tatizo la fangasi sehemu zao za siri wanaojulikana kama kandida.

Fangasi hawa wanapompata mwanamke wanamsababishia adha kubwa, kwani asipopata tiba anaweza kupata tatizo la kutokwa majimaji meupe au yenye rangi kama ya udongo na yenye harufu mbaya.

Tatizo hilo pia linaweza kuwapaa kinamama wanaotumia vipodozi vilivyopigwa marufuku na madaktari au kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.

Hali kadhalika wanaume nao wanaweza kupata tatizo hilo lakini wao halijitokezi isipokuwa huwaambukiza wanawake wanapojamiiana nao.

Ili kuondokana na tatizo hilo chukua limau moja changanya katika nusu lita ya maji kisha jisafishe sehemu zako za siri jifute na kupaka asali badala ya mafuta.

Fanya hivyo kwa muda wa wiki mbili hadi tatu tatizo hilo litakwisha kabisa. Tatizo hili lisipotafutiwa ufumbuzi kwa mjamzito mimba inaweza kutoka.

Wakati unatumia dawa hiyo na hata baada ya hapo hakikisha unafua chupi yako kwa maji moto au piga pasi kabla ya kuivaa, kunywa maji mengi, acha kutumia vinywaji vyenye sukari nyingi.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment