Saturday, 26 May 2018

Wajua mizizi, ndevu na majani ya mahindi ni dawa?


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallaha MandaiMAHINDI ni zao maarufu hapa nchini kwa kuwa yanastawishwa kwenye mikoa yote. Ni zao la chakula na biashara.

Umaarufu mkubwa wa zao hili ni kwa sababu ndilo chanzo kikuu cha unga wa kupikia ugali unaotumiwa na makabila mengi kama chakula kikuu.

Leo nauzungumzia mmea huu katika upande mwingine wa tiba. Kuanzia majani hadi mizizi, mhindi ni tiba ya magonjwa mengi.

Majani na mizizi ya mahindi vinatibu figo na kibofu cha mkojo, ndevu zake ni dawa ya maumivu wakati wa kukojoa, zinasaidia pia uvimbe wa miguu, wanaopata shida wakati wa kukojoa hususan wazee na watoto wanaokojoa kitandani pia ni tiba nzuri kwao.

Namna kuandaa

Chukua mizizi na majani, vitie katika maji vichemshe kwa muda wa dakika 15, chuja na kunywa.

Chukua ndevu za mahindi za kutosha, chemsha katika maji ya lita mbili muda wa dakika 15, chuja kunywa glasi mbili kwa siku, muda wa siku tano.

Unaweza pia kutumia kijiko kimoja cha mezani cha kitunguu maji kilichosagwa kuwa kama ujiuji, changanya na asali kijiko kimoja cha chai, kula mara tatu kwa siku kwa muda wa mwezi mmoja na nusu (majuma sita) ni dawa nyingine nzuri ya kutokojoa kitandani.

Mahindi yanayostawishwa shambani.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment