Tuesday, 29 May 2018

Waziri Ummy atoa futari kwa taasisi 10 za jiji la Tanga

Sehemu ya wakuu na wawakilishi wa taasisi mbalimbali
jijini Tanga wakimsikiliza  Waziri Ummy kabla ya kupokea
futari.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika halfa hiyo baada ya  kuwakabidhi  kila taasisi  futari yao.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (
katikati) 
akimkabidhi futari mmoja wa walezi wa vituo vinavyolelea watoto 
wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Tanga.  Vyakula ambavyo 
vimetolewa naye 
kwa kila taasisi imepata unga wa ngano kilo 
50, mchele kilo 100, sukari kilo 25,tambi mifuko miwili, mafuta ya kula lita 
20, maharage kilo100, unga wa dona kilo 25 na majani ya chai kilo 3, vyote 
vikiwa na thamani ya sh.milioni 6.8.

Ustadhi wa madrasa ya Zaharau, Ustadhi Abduswamad Muhammad akiomba dua kumshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia futari hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali mara baada ya kuwakabidhi futari.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akigawa futari kwa wawakilishi wa vituo mbalimbali na taasisi za kidini tano zilizopo jijini Tanga.
Sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa kwa ajili ya futari kwa taasisi 10 za mkoa wa Tanga ikiwemo magareza iliyotolewa na  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akimkabidhi futari Mkurugenzi wa taasisi ya kulea watoto wanaoishi kwenye Mazingira
magumu ya Goodwill,  Sayyed Muhdhar Idarus ambapo taasisi 10 zilinufaika na mgawo huo.


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kupitia Taasisi yake ya Odo Ummy Foundation jana amegawa futari kwa taasisi za kiislamu na magereza zilizopo jijini Tanga ili viweze kuwasaidia wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Vyakula ambavyo vimetolewa na ni unga wa ngano kilo 50, mchele kilo 100, sukari kilo 25, tambi mifuko miwili, mafuta ya kula lita 20, maharage kilo 100, unga wa dona kilo 25 na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 6.8.

Akizungumza baada ya kukabidhi futari hizo, mapema jana kwa taasisi zenye wanafunzi walitoka maeneo mbalimbali na wakati mwingine wanakuwa hawana uhakika wa kufuturu.

Amesema ameona atoe futari hiyo kwa kila taasisi badala ya kuwaita pamoja kufuturu nao maana wengine wanaweza kushindwa kupata fursa ya kuhudhuria.

“Nimeona ni bora nitoe futari hii badala ya kwenda kufuturu kila mahali kwani tutakapofanya hivyo wanaweza kuja wachache na mimi kutokana na kuwa nimetoka kwenye familia ya watu wa kawaida maskini nimeona angalu hicho kidogo ambacho nimejaliwa nitoa kwa taasisi za dini na watoto kwenye mazingira magumu,”amesema.

Ameongeza kuwa ameamua kufanya hivyo kwa taassisi hizo ambazo wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali ambao wamejifunza dini na vituo vinavyolea watoto kwenye mazingira magumu ili wakati huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani waweze kutimiza nguo hiyo muhimu ya funga bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ile.

Hata hivyo, ametoa mwito kwa watu mbalimbali kujitokeza kusaidia watoto yatima yanaolelewa kwenye vituo mbalimbali na taasisi za kidini kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ili waweze kupata uhakika wa kupata mahitaji yao muhimu wakati wa kufuturu.

Akizungumza baada ya kupokea futari hiyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Goodwil inayolea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, Sayyed Muhdhar amemshukuru Waziri Ummy kwa kuwapatia msaada huo wa futari ambao utakuwa chachu ya kuweza kuondoa changamoto ambazo wanakabiliana nazo hasa kipindi hiki cha funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amesema kitendo kilichofanywa na Waziri Ummy sio jambo dogo ni kubwa kutokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hususan kwenye
kipindi hiki cha mfungo kutokana na mahitaji kuongezeka.

“Namuomba Mwenyezi Mungu ampe nguvu na kumjalia maisha marefu na pale alipotoa aweze kuongezewa," amesema (Habari kwa Hisani ya Glob ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments:

Post a Comment