Saturday, 19 May 2018

Waziri Ummy Mwalimu azindua madarasa shule ya msingi Bombo

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi huo wa madarasa na makabidhiano kwa halmashauri ya jiji la Tanga.




Mstahiki meya wa jiji la Tanga, Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kushoto  ni katibu tawala wa wilaya ya Tanga (DAS), Faidha Salimu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza kwenye halfa hiyo kushoto  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bombo, Denis Mushi akizungumza wakati wa halfa hiyo.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizindua madarasa ya shule ya msingi Bombo, jijini Tanga.  Kushoto ni mstahiki meya wa jiji la Tanga, Alhaj Mustapa Selebosi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifungua mlango mara baada ya kuzindua  madarasa ya shule ya msingi Bombo. Kushoto ni mstahiki meya wa jiji la Tanga, Alhaj Mustapa Selebosi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiingia ndani ya madarasa mara baada ya kuyazindua, kulia kwake  ni mstahiki meya wa jiji la Tanga, Alhaj Mustapa Selebosi.

Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi Mayeji (kulia) akimwonesha kitu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kabla ya kuzindua madarasa ya shule ya msingi Bombo, ya jijini Tanga. Kushoto ni mstahiki meya wa jiji hilo, Alhaj Mustapa Selebosi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kulia) akifurahia jambo na Meya Alhaji Mustapa Selebosi mara baada ya kuzindua madarasa ya shule ya msingi Bombo.

Sehemu ya wananchi na viongozi waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia matukio mbalimbali.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jami,i Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha akiwa amekalia madawati mara baada ya kufanya uzinduzi huo.

Kundi la Wasanii la Tanga Kwanza likitumbuiza kwenye uzinduzi huo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa nne kushoto), akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua madarasa hayo kushoto ni meya wa jiji la Tanga, Alhaji Mustapha Selebosi kulia mwenye suti ni mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi Mayeji.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Bombo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wanaounda kundi la Tanga Kwanza.


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali kila mwezi imekuwa ikitenga sh.milioni 55 kwenye jiji la Tanga kwa ajili ya shule za msingi  ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila vikwazo na hivyo kupata elimu bora.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11 kwenye shule ya Msingi Bombo kwenye halmashauri ya jiji hilo ambavyo ujenzi wake umedemu kwa muda wa zaidi ya mwaka mmojana kugharimu  zaidi ya sh. milioni 279 zilizotokana na mapato ya ndani.

Ndani ya kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule ya Msingi Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao uliathiri taaluma yao.

Waziri Ummy amesema licha ya hivyo lakini pia serikali imekuwa ikitenga sh.milioni 108 kwa ajili ya shule za sekondari kwenye jiji hilo ili kuhakikisha wanaweza kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili kupitia sekta hiyo.

“Ndugu zangu ninafuraha leo kufungua madarasa haya ambayo yamejengwa kwa kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila vikwazo lakini pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali inaleta milioni 55 kila mwezi kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia naahidi kushirikiana nanyi.

“Lakini pia kadri tunavyoacha kwenda Marekani na Ulaya ndivyo fedha hizo zinasaidia kutumika kwenye harakati za kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuwapa watoto wetu elimu bora,”amesema.

Awali akizungumza katika ufunguzi huo, meya wa jiji la Tanga,  Alhaji Mustapha Selebosi amempongeza, Rais Dk. John Magufuli kupitia Wizara ya Elimu kwa kuweka msukumo ambapo aliahidia kuzungumza na waziri wa wizara hiyo kuweka mradi wa matokeo kwanza ndio wakapata na kupokea sh. milioni 136.6.

“Katika suala hili naomba nikupongeze Waziri Ummy kwa kulipigania jiji la Tanga ndani na nje ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hivyo nisema tutaendelea kushirikiana,”amesema.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bombo, Denis Mushi aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano  kwa kuhakikisha ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati ili wanafunzi waendelee vizuri na masomo.  (HABARI KWA HISANI YA GLOB YA KIJAMII YA TANGA RAHA)

No comments:

Post a Comment