Sunday, 10 June 2018

Chenza tunda tamu lenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu


Chenza lililowiva

CHENZA ni tunda jamii ya chungwa. Licha ya kuwa maeneo mengi yanayostawishwa machungwa, machenza nayo hupatikana lakini si mengi kama machungwa.

Kama mara nyingi ninavyozungumza katika mada zangu mbalimbali kuwa ukimwuliza mtu kwanini una kula chenza atakuambia kwa kuwa ni tunda tamu lakini hawezi kukuambia faida zilizomo ndani ya tunda husika.

Tunda hili tamu lina faida nyingi sana katika mwili wa binadamu ikiwemo kuongeza vitamin C, linazuia kuvuja damu katika fizi, lina imarisha mifupa, linaongeza nguvu katika miusuri nakuondoa maumivu ya viungo.

Pia linaondoa baridi yabisi, linaondoa viuvimbe chini ya tumbo, linasaidia kuondoa mawe katika figo na kibofu, linatibu unene na mirija ya damu na kutibu udhaifu wa macho.

Kula tunda lenyewe lililowiva tu. Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga, Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745 900 600 pia unaweza kutembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

3 comments: