Saturday, 9 June 2018

Hii ndiyo siri ya mnanasi ni tiba ya maradhi tishio


Mnanasi
NANASI ni tunda la msimu linalopendwa na wengi kutokana na ladha yake tamu ya sukari. Nanasi linazaliwa kutokana na mmea unaojulikana kama mnanasi.
Radha nzuri ya nanasi lililowiva inaliongezea umaarufu tunda hilo kila kukicha na hivyo idadi ya wapenzi wake kuongezeka kila leo. Nanasi linaliwa kama tunda huku wengi wakipendelea juisi yake tamu.
Wakati mwingine nanasi bivu linachanganywa na parachichi ama embe kupata juisi yenye radha tamu zaidi. Tunda hili pia ni chanzo muhimu cha vitamini na madini ambayo yanasaidia kuimarisha afya ya mwanadamu.
Wakati wengi wakipanda mmea huu ili uzae matunda kwa ajili ya familia na biashara, mnanasi ni tiba nzuri sana kwa maradhi mengi. Majani ya nanasi yanatumika kwa wenye matatizo ya afya ya akili, kama kusahau na kuchanganyikiwa.
Matatizo hayo pamoja na mambo mengine yanababishwa na ubongo kutopata chakula chake ipasavyo kwa maana ya hewa ya oksjeni.
Kutumia tiba hii chukua majani ya mnanasi kata vipande vidogo, kisha vitwange na kuchemsha kwa muda wa dakika 15 kisha kunywa maji yake kwenye kikombe cha chai asubuhi na jioni.
Majani haya pia yanasaidia kurudisha madini ya chuma kwa wenye tatizo hilo.
Mizizi ya mnanasi pia inasaidia sana kwa kinamama wenye tatizo la maziwa kuuma, maumivu ya mgongo na afya ya uzazi ambapo tiba hii uwezo mkubwa wa kupevusha mayai.
Kunywa dawa hii mara mbili kutwa asubuhi na jioni muda wa siku 15. Juisi ya nanasi bichi nayo ina nguvu ya kuimarisha afya ya ubongo kwa kuwa na kumbukumbu nzuri. Juisi ya nanasi lililowiva inasaidia mmeng’enyo mzuri wa chakula tumboni.
Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 pia tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment