Monday, 11 June 2018

Huu ndiyo mpapai tunda na tiba ya magonjwa mengi

Mpapai

UMAARUFU wa mpapai unatokana na mmea huo kuzaa mapapai ambayo ni matunda matamu sana yanayopendwa na kuliwa na wengi.

Wakati mpapai ukijipatia umaarufu kwa sababu tu ya kutoa matunda matamu, wataalam wa tiba asili wamebaini maajabu mengine makubwa ya kitiba yaliyosheni katika mmea huu.

Tukianzia na papai lililowiva limesheni vitamin A, B, C, D na E ambapo likiliwa pamoja na mbegu zake linasaidia kuondo shida ya kusaga chakula tumboni, udhaifu wa tumbo, kisukari na athma, linachochea afya nzuri kwa mtumiaji ikiwa ana lila kila siku na pia linatibu kiungulia.

Papai pia linatibu mahali palipoungua moto, linasaidia kutofunga choo, linaondoa tatizo la njia ya haja kubwa kwa ndani, maganda yanasaidia kuondoa vipele na saratani ya ngozi pia mgonjwa wa kifua kikuu akila tunda hilo kwa muda mrefu anaweza kupona bila kutumia dawa nyingine.

Mizizi ya mpapai iliyochemshwa inasaidia tatizo la figo zinazovuja, inaua minyoo tumboni, inatibu meno ikiwa unachanganya na miche mingine, mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji lita mbili na kuchemshwa kwa muda wa dakika 15 yanatibu figo, kibofu cha mkojo na kuzuia kutapika.

Majani mabichi ya mpapai huwekwa juu ya vidonda na shida ya ngozi, majani yake yakikaushiwa ndani, yanatibu pumu, inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize kule kubanwa kutakwisha.

Majani yake mabichi yanasaidia shinikizo la damu, yaloweke katika maji moto na kunywa kikombe kimoja kutwa mara mara tatu pia maziwa yatokayo katika jani la mpapai huponya vidonda.

Maua ya mpapai yakilowekwa katika maji moto na kuongeza asali kidogo ni tiba ya mafua na kikohozi kitokanacho na mapafuni na kifua kikuu.

Mbegu za papai zilizosagwa ni dawa ya minyoo, mbegu zilizokushwa ndani kisha kusagwa kuwa unga unatibu malaria ambapo tumia kijiko kimoja cha chai changanya katika uji, kunywa mara tatu kwa muda wa siku tano.

Mada hii imeletwa kwako nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 pia tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi kuhusua masuala ya kiafya.

1 comment: