Thursday, 7 June 2018

Kanali Hawa awataka wahitimu JKT kudumisha nidhamu, uzalendo


Kanali Hawa Kodi

Wankyo Gati, Arusha

MKUU wa tawi la utawala kutoka Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Kanali Hawa Kodi amewataka vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT kutambua na kuzingatia madhumuni ya kuanzishwa kwa jeshi hilo.

Malengo hayo ni pamoja na kuwaandaa kuwa na nidhamu na uzalendo kwa nchi pamoja na kujituma katika shughuli za kujenga taifa.

Kanali Kodi ametoa kauli hiyo wakati wa kufunga mafunzo ya JKT kwa vijana 360 waliohitimu katika kikosi cha 839 KJ Makuyuni, wilayani Monduli, mkoa wa Arusha.

Amesema mafunzo ya JKT yana umuhimu mkubwa kwa vijana wa sasa kutokana na mwingiliano wa tamaduni unaosababishwa na utandawazi.

Ameongeza kuwa  katika kipindi cha utandawazi maadili ya vijana yameingiliwa na tamaduni sizizo na maadili hivyo wanapaswa kuwa mfano wa kuibadilisha jamii.

Kwa upande  wao vijana hao wanasema wameandaliwa na kuiva vema baada ya kupata mafunzo mbalimbali, huku kaimu kamanda wa kikosi 839 KJ Makuyuni Luteni kanali Festo Mbanga akithibitisha kwa kutaja kozi walizopitia.

Naye mkuu wa wilaya ya Monduli, Idd Kimanta, ambaye ndiye aliyefunga mafunzo hayo amewakumbusha wahitimu hao kuzingatia kiapo na mafunzo waliyopata.

Amewataka kuwa wazalendo na kulinda nchi yao kwa kuhakikisha mafunzo hayo hayatumiki kinyume na lengo.

No comments:

Post a Comment