Saturday, 9 June 2018

Kikwete ataka CMSA kutoa elimu ya ununuzi wa hisa kwa watanzania

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akigonga kengele kuashiria kurudishwa rasmi kampuni ya Nicol katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).


Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama akitoa maelezo kwa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuhusu kuingia Nicol kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa bodi ya Nicol, Dk. Gideon Kaunda akitoa maelezo kwa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuhusu kuingia Nicol katika soko hisa na changamoto walizofanikiwa kukabiliana nazo.


Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili Nicol kwa mara nyingine


Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili Nicol kwa mara nyingine


Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ameishauri Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), kutoa elimu kwa watanzania kuhusu ununuzi wa hisa katika soko la hisa.

Kikwete ameyasema wakati wa hafla ya Kampuni ya Nicol kurudishwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), baada ya kukidhi vigezo vya kisheria vinavyoiruhusu kuingia katika soko hilo.

Amesema CMSA ikitoa elimu kwa wananchi itasaidia kuongeza hamasa ya ununuaji hisa kuliko ilivyo sasa.

Rais huyo mstafu amesema CMSA ikifanya ikifanya hivyo kampuni nyingi zitaorodheshwa katika soko la hisa na hivyo kuongeza uwekezaji wa miradi mingine.

Aidha, amesema kutokana na ukuaji wa teknolojia katika masoko CMSA imeshauriwa kuboresha zaidi mnada wa soko la hisa wakati wa kufungua na kufunga.

"Nakumbuka wakati serikali inauza hisa zake NMB kulikuwa na mjadala mkali wa kuhoji kwanini Nicol wapewe asilimia tano, lakini kwa imani kwamba hii ni kampuni ya wazalendo, basi tukachukua uamuzi kuwapa wazalendo," amesema na kuongeza.

Naye kaimu ofisa mtendaji mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama, amesema mamlaka hiyo imefanikiwa kuorodhesha hisa 69,165,170 za Kampuni ya Nicol katika DSE baada ya kukidhi vigezo vya kisheria.

Amesema Nicol iliondolewa katika orodha ya kampuni zilizoorodheshwa DSE Juni 2011 kutokana na matatizo ya kiutendaji katika uwekezaji.

No comments:

Post a Comment