Thursday, 7 June 2018

Maji yanavyosaidia kutibu miguu kuwaka motoMIGUU kuwaka moto ni mwiba unaowakwaza waathirika wa tatizo hilo kwani hujikuta kukosa raha kutokana na maumivu wanayokabiliana nayo hivyo kuhitaji tiba ya uhakika.

Hata hivyo, jambo la kutia moyo ni kwamba tatizo hilo linaweza kwisha iwapo utazingatia maelekezo ya kitaalam kwa kutumia maji moto.

Chukua maji moto, joto lisiwe la kuunguza, weka maji hayo katika beseni kiasi cha kupita ugoko kwa maana ya juu ya kisigino, weka mguu mmoja na mwingine weka katika maji baridi ya kawaida.

Miguu ikae muda wa dakika 15 badilisha, ule uliouweka katika maji moto uweke katika baridi na wa maji baridi weka katika moto, badilisha na maji pia.
Zoezi hili lifanye kwa muda wa siku 15, utaona mabadiliko makubwa katika miguu yako yenye maumivu.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment