Sunday, 10 June 2018

Manji ahudhuria mkutano mkuu wa Yanga


Yusuf Manji


Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA mwenyekiti wa Klabu ya Yanga African na mfanyabiashara maarufu, Yusuph Manji ni miongoni mwa watu maarufu wanaohudhuria mkutano mkuu wa klabu hiyo leo.

Mkutano huo unafanyika kwenye ukumbi wa Police Officers Mess, Oyster Bay, Dar es Salaam, kuanzia saa 3 asubuhi.

Taarifa zinasema Manji, amekubali kuhudhuria mkutanoni ili kujumuika na wanachama wa klabu hiyo.

Mkutano huo unafanyika huku malengo makubwa yakiwa ni kubadilisha mfumo wa uendeshwaji wa klabu hiyo kutoka unaotegemea wanachama na badala yake kuwa wa uwekezaji.

Licha ya Manji, waziri mwenye dhamana ya michezo, Harrison Mwakyembe naye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi baada ya kualikwa na viongozi wa Yanga.

Awali uongozi wa Yanga uliwaomba wanachama kufika mkutanoni wakiwa na kadi zao zikiwa hai ili kuweza kuingia ukumbini.

No comments:

Post a Comment