Sunday, 10 June 2018

Mlingoti mti wenye maajabu katika tiba


MITI mingi tunaipanda katika nyumba zetu ili kuzinadhifisha  na kutupatia kivuli. Miti hiyo karibu yote ni dawa nzuri sana lakini wengi wetu hatujui.

Mlingoti ni mti mrefu ambao kama nilivyosema ukipandwa jirani na nyumba unaifanya nyumba yako kuonekana maridadi, lakini faida ya mti huo ni zaidi ya hiyo kwani ni dawa ya magonjwa mengi.

Mti huo unaweza kutibu athma, matezi, kibofu cha mkojo, kifua kikuu, kifua cha mapafu, kuoshea vidonda, kukanda katika viungo vyenye maumivu na uvimbe, kuulia wadudu, kikohozi kikavu, kisukari, malaria na figo.

Pia unasaidia kuondoa maumivu ya viungo, baridi yabisi, kuhara damu, maradhi ya kinywa, kuungua moto na mafua ambapo unatakiwa kuchemsha majani ya mlingoni kisha vuta mvuke wake.

Namna ya kuandaa; chukua majani ya mlingoti yenye uzito wa gram 30 yaoshe vizuri kisha tia lita moja ya maji moto, kunywa glasi moja kutwa mara tatu.
Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga, Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745 900 600 pia unaweza kutembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment