Thursday, 7 June 2018

Mwigulu ataka msongamano magerezani umalizwe


Dk. Mwigulu Nchemba

Wankyo Gati, Arusha

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Jeshi la Magereza nchini linakabiliwa na changamoto ya msongamano mkubwa wa mahabusu hususan kwenye magereza ya mijini.

Kutokana na changamoto hiyo serikali inakusudia kuwahamishia wafungwa kwenye magereza ambayo yana wafungwa wachache yaliyoko pembezoni ili kupunguza msongamano.

Ili kufanikisha jitihada hizo amelitaka Jeshi la Magereza kubainisha magereza yenye shughuli za uzalishaji ambayo yana upungufu wa nguvu kazi ili waweze kuwapeleka huko kuongeza nguvu katika maeneo hayo. 

Waziri Nchemba amesema hayo baada ya kutembelea Gereza kuu la mkoa wa Arusha kusikiliza changamoto zinazowakabili ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais la kushughulikia kero zilizopo magerezani.

Amesema kuna magereza katika maeneo mbalimbali yenye shughuli za uzalishaji ambayo kama yatapelekewa nguvu yataweza kusaidia jeshi hilo kupunguza utegemezi.

Naye Mkuu Jeshi la Maereza, mkoa wa Arusha, Kamishna msaidizi mwandamizi Hamisi Nkubasi amesema magereza ya maeneo mbalimbali yenye maeneo makubwa ya kilimo yakipewa kipaumbele yataweza kutatua changamoto ya chakula kwa jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment